×

Scrub ya sukari, kahawa na mafuta ya mzaituni kwa ngozi ya mwili

Watu wengi wana uchafu kwenye ngozi hata wakioga bila kujua sababu ni nini, wengine wanakuwa na weusi f,lani hata kama ni mweupe. Utasikia mtu anasema f’lani haogi vizuri, siyo kweli ni ngozi inakuwa imechoka.

Scrub nzuri ya kuondoa weusi huo ni sukari na  mafuta ya mzaituni ambayo inapakwa kisha unafanyia masaji mwili mzima kuondoa uchafu wa ngozi.

Jinsi ya kuandaa

Chukua kahawa vijiko viwili vikubwa, kijiko 1 kikubwa cha sukari na mafuta ya mzaituni vijiko vinne. Changanya vyote kwa pamoja upate mchanganyiko.

Baada ya hapo, chukua mchanganyiko huo paka mwilini mwako, ufanyie mwili masaji kama unayesugua sehemu hasa sehemu nyeusi, zoezi hilo lifanye wakati unaoga.

Nikisema sehemu nyeusi namaanisha kwenye maungio, makwapani na shingoni, hizi ni sehemu ambazo weusi wake huwa unazidi hivyo kwa kutumia mchanganyiko huu unaweza kurudisha rangi asili ya ngozi yako.

Kwa wanaotaka kung’arisha miguu scrub hii pia ni nzuri, inafaa kwa asilimia kubwa. Scrub hii inafaa kwa sehemu yote ya mwili isipokuwa usoni tu.

Leave a Comment