
Mechi hii ya kihistoria inachezwa leo Uwanja wa Old Trafford kuanzia saa 17:30 jioni, huku timu zote zikiwa zimetofautiana kwa pointi 3 tu na tofauti ya magoli pamoja na Aston Villa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kumaliza kwenye nafasi tatu za juu.
United wakiongozwa na kocha wa muda Michael Carrick wamekuwa wakiimarika hivi karibuni, huku Liverpool wakiwa na presha kubwa baada ya kufungwa mabao mengi na Manchester City na PSG hivi karibuni. Timu zote mbili zina kisasi,
Liverpool wanalenga kulipiza kulipa kipigo walicho kipata kutoka kwa United mwezi Oktoba mwaka jana Anfield, huku United wakitaka kuthibitisha ubora wao wakiwa nyumbani baada ya kunyang’anywa ushindi wa 3-0 msimu uliopita uwanjani kwao.
Kocha Michael Carrick anaweza kuwa na mkakati unaomtegemea Bruno Fernandes kiungo na Benjamin Sesko mbele, huku kocha wa Liverpool Arne Slot akihitaji kuwa na uthabiti wa safu ya ulinzi ili kuepusha makosa yaliyojirudia kwenye mechi za hivi karibuni.
Kwa Slot, mechi hii ni mtihani wa ukomavu wa timu yake baada ya kukosolewa kwa kutokuwa na utambulisho wa kikosabahi, huku Carrick akijaribu kujiimarisha zaidi kwenye nafasi yake ya muda kabla ya kumaliza msimu kwa matokeo chanya.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
United watawakosa nyota wao muhimu kama vile Matheus Cunha aliye na jeraha la nyonga, na hali ya Luke Shaw haijulikani baada ya kuondolewa kwenye mchezo dhidi ya Brentford.
Kwa upande mwingine Liverpool wanakosa nyota wao mkubwa Mohamed Salah kwa jeraha la paja, pamoja na Hugo Ekitike, Conor Bradley na kipa wao Alisson berka ambaye bado hajathibitishwa kurejea. Katika upande wa United, Leny Yoro amerejea kwenye kikosi, huku Benjamin Sesko akitegemewa kuwa tishio la mabao, wakati Liverpool wakimtegemea Alexander Isak na Florian Wirtz kuleta mabadiliko mbele ya lango bila Salah na Ekitike.
Kwa kuzingatia United wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na ari ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Brentford na kushinda Chelsea ugenini, wanaweza kutumia faida ya nyumbani na kutokuwa na wachezaji wao wa kwanza kwa Liverpool kupata angalau sare au ushindi. Wakati huohuo, Liverpool wakimkosa Salah, shinikizo lao la ushindi ni kubwa ili kusalia kwenye mwendo wa kufuzu Michuano ya Ulaya, hivyo wanajiandaa kwa bidii japo wakumbukumbu ya kufungwa na Brighton ugenini inawafanya wawe waangalifu. Jisajili