×

Mwili wa James Temba Kusafirishwa Kwenda Moshi kwa Mazishi – Video

Baba wa kijana James Temba ambaye inadaiwa aliuawa kisha mwili wake kukatwa kichwa, amesema mwili wa marehemu mwanaye utasafirishwa kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

Akizungumza na Global TV, Temba ameeleza kuwa mambo yakienda sawa, Jumatano Mei 6, 2026 mwili utapelekwa katika Kanisa la KKKT Tabata kwa ajili ya ibada ya kuaga kisha utasafirishwa kwenda Moshi.

Mwili wa James ulikutwa kwenye Mto Msimbazi, eneo la Kipawa, Ilala jijini Dar es Salaam ukiwa umekatwa kichwa, tukio lililoibua simanzi kubwa.

Video kamili ipo Youtube, Global TV.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

Leave a Comment