×

Godbless Lema: Maridhiano ya Kweli Si Kumtoa Tundu Lissu Gerezani Pekee – Video

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa maridhiano ya kweli nchini hayawezi kuwa suala la kumtoa Tundu Lissu Gerezani pekee, bali ni kurudisha Taifa katika misingi ya sheria, haki na utaratibu ili kila Mwananchi aweze kupata haki yake bila upendeleo.

Lema ameyasema hayo leo Mei 08, 2026 Jijini Arusha wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Soko Kuu Arusha mbele ya Wanachama na wafuasi wa CHADEMA, ambapo alizungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa na hali ya demokrasia Nchini huku akisisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya Katiba na utawala wa sheria.

 

Leave a Comment