Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, ameipongeza Serikali akisema kuwa sekta ya afya nchini imepiga hatua kubwa tangu Tanzania ipate uhuru.
Shigongo amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala, ambapo alieleza tofauti ya huduma za afya kati ya kipindi cha baada ya uhuru na hali ilivyo sasa.
Mbunge huyo alitumia takwimu mbalimbali kuonyesha maendeleo yaliyofikiwa katika huduma za afya, miundombinu ya hospitali pamoja na upatikanaji wa huduma za matibabu nchini.