×

Waziri Mkuu Mwigulu Awakilisha Tanzania Mkutano wa Afrika na Ufaransa Nairobi

Dkt. Mwigulu Nchemba leo Mei 12, 2026 amemuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa unaofanyika jijini Nairobi.

Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu alionekana akisalimiana na Dkt. William Ruto wakati wa mkutano huo unaojulikana kama Africa Forward Summit: Africa-France Partnership for Innovation and Growth.

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji na wadau mbalimbali kujadili ushirikiano wa maendeleo, ubunifu, uwekezaji na ukuaji wa uchumi kati ya mataifa ya Afrika na Ufaransa.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unaonyesha dhamira ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika maeneo ya biashara, teknolojia na maendeleo endelevu.

Leave a Comment