Rais Samia Ahudhuria Sherehe za Kuapishwa kwa Museveni Uganda (Picha +Video)
Global Publishers May 12, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwenye hafla ya Uapisho wa Rais huyo iliyofanyika katika Viwanja vya Kololo, Kampala nchini humo tarehe 12 Mei, 2026.
Rais Samia Suluhu Hassan, ameshiriki sherehe za uapisho wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, uliofanyika leo, Mei 12, 2026 jijini Kampala, Uganda.
Mbali na Rais Samia, Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine mbalimbali wamehudhuria uapisho huo.
Museveni ameapishwa rasmi kuanza muhula wake wa saba kama rais wa Uganda hatua inayohitimisha miaka 40 kamili tangu aingie madarakani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda tarehe 12 Mei, 2026. Rais Dkt. Samia amewasili nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, zinazofanyika katika Viwanja vya Kololo Jijini Kampala nchini humo.