×

Mo Dewji Akutana na Wachezaji wa Simba Kuwapa Hamasa

Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji maarufu kama Mo Dewji, leo amekutana na kufanya mazungumzo na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa kuelekea michezo ya mwisho ya msimu.

Katika kikao hicho, Mo Dewji aliwataka wachezaji waendelee kupambana kwa kujituma ili kuhakikisha timu inamaliza msimu kwa mafanikio huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano, nidhamu na kujitolea ndani na nje ya uwanja.

Aidha, Rais huyo wa Simba alieleza imani yake kwa kikosi hicho pamoja na benchi la ufundi akiamini kuwa timu ina uwezo wa kufanya vizuri katika mechi zilizobaki msimu huu.

Kwa upande wao, baadhi ya wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi walieleza kufurahishwa na sapoti pamoja na hamasa kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo wakiahidi kupambana kwa nguvu zote ili kufikia malengo ya timu.

Simba SC inaendelea na maandalizi ya michezo yake ya mwisho ya msimu huku mashabiki wa klabu hiyo wakiendelea kuwa na matumaini ya kuona timu yao ikifanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

ALLY KAMWE AFUNGUKA ISHU YA MWAMNYETO KUTO KUWA SAWA – ”MASHABIKI WAUNGANE KUMUOMBEA”…

Leave a Comment