×

Rais Samia Aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia Oktoba 29

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo imechukuliwa katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais iliyochunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea kipindi cha uchaguzi huo, kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.

Katika uteuzi huo, Shabani Ally Lila ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Wajumbe wengine walioteuliwa kuwa makamishna ni pamoja na Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir pamoja na Aishieli Nelson Sumari.

Tume hiyo inatarajiwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya ghasia yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

GERSON MSIGWA -“UNAKUTA MSANII ANAUMWA ANAKOSA PESA ya KUTIBIWA LAKINI KAZI ZAKE ZINATUMIKA”…

Leave a Comment