×

Rio Ferdinand Atembelea Bunge la Tanzania Katika Ziara ya Michezo na Utalii

Rio Ferdinand, Nahodha na Mchezaji wa zamani na wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, akiwa katika viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushuhudia shughuli za uendeshaji wa Bunge hilo, leo Mei 20, 2026 Jijini Dodoma, ikiwa ni muelendelezo wa ziara yake nchini Tanzania ambayo inalenga kuboresha sekta ya michezo pamoja kuona vivutio vya kitalii.

Rio Ferdinand, nahodha na mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza pamoja na Klabu ya Manchester United, leo Mei 20, 2026 ametembelea viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Bunge hilo.

 

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa safari yake nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha sekta ya michezo pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.

Katika ziara hiyo, Rio Ferdinand amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ambaye alikuwa mwenyeji wake katika shughuli hiyo muhimu.

Rio Ferdinand akiwa na wachezaji wa zamani wa Klabu za Tanzania na timu ya Taifa pamoja na wadau wengine wa soka kwenye viunga vya Bunge.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu akiwa na Mchezaji wa zamani na wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand kwenye viunga vya Bunge.
Spika Mussa Zungu akiwa na Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Mchezaji wa zamani na wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand pamoja na Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 (U20) Tanzanite Queens ambao wamefuzu kucheza Kombe la Dunia kwenye viunga vya Bunge hilo leo Mei 20, 2026 Jijini Dodoma.

Leave a Comment