
Msanii wa Afrika Kusini, Tyla, ameendelea kung’ara kimataifa baada ya kushinda tuzo ya Social Song of the Year kwenye tuzo za American Music Awards 2026 kupitia wimbo wake “CHANEL”.
Tuzo hizo zimefanyaika katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena, Las Vegas usiku wa kuamkia leo Mei 26, 2026. Mbali na ushindi huo mkubwa, Tyla pia alitwaa tuzo ya Best Afrobeats Artist, akithibitisha kuwa ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaotikisa zaidi duniani kwa sasa.
Nyota huyo aliingia kwenye tuzo hizo akiwa na jumla ya nominations nne, zikiwemo:
- Best Female R&B Artist
- Best Music Video
- Social Song of the Year
Mafanikio hayo yamemfanya Tyla kuwa msanii wa Afrika mwenye nominations nyingi zaidi katika historia ya American Music Awards.
Tangu kutolewa kwake Oktoba 2025, wimbo wa CHANEL umeendelea kufanya vizuri duniani baada ya kuvuka zaidi ya streams milioni 320 kwenye Spotify.
Aidha, Tyla pia ametajwa kwenye vipengele viwili vya BET Awards 2026, hatua inayoonyesha kuendelea kupaa kwa umaarufu wake kimataifa.
Katika tuzo hizo zilizofanyika mjini Las Vegas, mastaa wengine waliotamba ni pamoja na:
- BTS
- Sabrina Carpenter
- Bruno Mars
- KATSEYE
- HUNTR/X
Tyla anaendelea kuwa sura mpya ya muziki wa Afrika duniani huku mafanikio yake yakizidi kuwavutia mashabiki wengi kimataifa.