×

KCB Tanzania Yazindua Huduma ya KCB Lipa Kurahisisha Malipo ya Kidijitali

KCB Bank imezindua huduma mpya ya KCB Lipa kwa wafanyabiashara na wateja, hatua inayolenga kurahisisha malipo ya kidijitali nchini.

Katika uzinduzi huo, KCB Bank imesema huduma ya KCB Lipa inawawezesha wafanyabiashara wake kupokea malipo kutoka benki mbalimbali pamoja na mitandao ya fedha za simu, bila gharama za ziada.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkuu wa Huduma za Kifedha Kidijitali Priscus Kessy amesema mfumo huo ni sehemu ya mkakati wa kuboresha ujumuishi wa kifedha na kuongeza ufanisi wa malipo ya kidijitali kwa biashara mbalimbali.

Naye Meneja wa Benki Mtandaoni na Ubunifu Nelson Perez amesisitiza kuwa KCB Lipa inalenga kuleta ubunifu zaidi katika huduma za kibenki mtandaoni, hususan kwa kurahisisha miamala kati ya benki na mitandao ya simu.

Kwa kifupi: KCB Lipa inatarajiwa kuongeza kasi ya malipo ya kidijitali na kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara na wateja nchini.

Leave a Comment