Rais wa Tanzania Samia Apokelewa Kwa Heshima Urusi Katika Ziara ya Kitaifa (Picha +Video)
Global Publishers June 2, 2026 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, uliopo Jijini Moscow kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa, nchini Urusi tarehe 02 Juni, 2026. Ziara hii ina lenga kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kihistoria baina ya Tanzania na Urusi.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewasili nchini Urusi kwa ziara ya kitaifa inayotarajiwa kuanza rasmi Juni 3 hadi Juni 6, 2026, kufuatia mwaliko wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi, huku Rais Samia akitarajiwa kushiriki pia katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF).
Tazama mapokezi ya Rais Samia akiwa nchini Urusi kwa ziara hiyo ya kihistoria.
Rais Samia akiwa amesimama wakati akipokea heshima ya wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vnukovo, Jijini Moscow kwa ajili ya Ziara ya Kitaifa nchini Urusi tarehe 02 Juni, 2026.