×

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-8

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Hawezi bwana, basi sikia, nazima taa halafu nafungua mlango tunaanza yetu ili akija tumsikie kisha usimame kitandani na ujifanye unaweka balbu,” Aisha alitoa mwongozo…
JIACHIE MWENYEWE SASA…

“Mh! Hebu jaribu,” alisema Bony akiwa na wogawoga wa mbali. Ni baba mwenye nyumba ilikuwa lazima achukue tahadhari kubwa.
Aisha aliifuata ‘bediswichi’ na kuzima taa ya chumbani kisha akapata wazo jingine huku kukiwa na giza nene ndani, akamwambia Bony kwa sauti ya chini hivi…
“Mi naona tusimame kitandani wote, tumalizie mambo yetu hapa, ili kama anaingia ni rahisi kuwasha taa akajua umetengeneza.”
“Sawa, hiyo sawasawa,” alisema Bony huku akiwa tayaritayari kwa kuvua bukta nusu…
“Panda basi,” alisema Bony kumwelekeza Aisha ambaye alikuwa akitetemeka kwani kitendo walichokuwa wanadhamiria kukifanya ndani ya nyumba hiyo ni cha hatari kwa vile Neema alikuwa chumbani amelala.
Aisha alipanda kitandani, Bony naye akapanda, wakawa wamesimama juu ya kitanda ambapo walianza mechi hapohapo huku kukiwa na giza.
Aisha hakuwa na jinsi, alijitahidi ili kuhakikisha anakata kiu yake kwa wizi huo. Alijitahidi kusema maneno ya chini kwa chini lakini akiamini kuwa, Bony anasikia ila hayafiki chumbani aliko Neema.
Amani aliyokuwa nayo Bony ni kujua kwamba, mlango wa chumbani kwake una tabia ya kulia ‘mbaa’ unapofunguliwa hali ambayo lazima ingemshtua pale uwanjani alipo na kuachana na mchepuko kushughulikia taa au balbu.
Ilifika mahali Aisha alishindwa kuvumilia, akajikuta akianguka kitandani puu na Bony akafuata haraka sana maana naye alikuwa kasi, wote wakawa puuu..!
Licha ya kuanguka, waliendelea na mechi huku Aisha akijiachia kama vile yuko kwake na mumewe, Mudy maana tukelele sasa tulianza kuwa juu, Bony akawa anamfumba kinywa kwa kiganja.
Ilikuwa wakati Aisha ameshatangaza nia, Bony akamruhusu maana si alishatoka uwanjani muda mfupi nyuma, wakasikia mbaaa! Ule mlango wa chumbani kwa Neema.
Bony alijinasua akisema…
“Neema anakuja baby.”
Aisha alimbana sana maana alikuwa katika hali tofauti na kawaida, akambana vilivyo huku akitaka kusema lakini akashindwa. Kama si jitihada za Bony kumtoa kwa nguvu, wangenaswa.
Palepale Bony alisimama huku Aisha akiwa bado amelala na kujinyoosha, akakurupuka na kusimama katikati ya chumba…
“Pole mamy, taa bado?” aliuliza Neema akiwa ameingia baada ya kuukuta mlango uko wazi.
Bony alisimama akiwa anashikashika balbu kiaina ili aonekane anashughulikia kweli…
“Mwaya we! Nimechoka na kuchoka, afadhali hata angefanya kesho kumbe,” alisema Aisha kwa sauti huku moyoni akisema…
“Nilichotaka nimepata, yaani we ulitaka ule wewe tu mimi nilale nahesabu paa…aaah! Wapi!”
“Aaah! Yaani ililegea, nimejaribu kuibanabana halafu sina vifaa…hebu jaribu kuiwasha kwanza,” alisema Bony.
Neema kwa sababu alisimama mlangoni ikawa rahisi kwake kuwasha taa ya bediswichi maana kamba yake ilikuwa ikining’inia jirani na sehemu ya kichwani ya kitanda hicho, taa! Taa ikawaka, maana yake Bony alifanikiwa kutengeneza.
Bony aliruka chini, akasimama kuiangalia balbu…
“Nadhani haiwezi kuzima tena shemeji,” alimwambia Aisha…
“Eee! Lakini hata ikisumbua sasa itakuwa kesho. Kwanza nakushukuru kwa kujitolea kuja kunitimizia matakwa yangu, maana ungeweza kusema umechoka, uko na mamaa,” alisema Aisha lakini kama alikuwa na maana nyingine ambayo Neema hakuielewa.
Aisha alimshukuru Bony kwa kwenda kumkata kiu japokuwa alikuwa na mkewe, Neema kule chumbani…
“Huyu ana ubavu wa kuacha kukutimizia unachotaka? We hujui kama nyumba ndogo zinajaliwa sana?” alisema Neema akitania huku akitangulia kuondoka…
“Umeonaee?” alisema Aisha akimwangalia Bony kwa jicho la mahaba.
Bony naye akaaga kuondoka…
“Basi usiku mwema shemeji, ikisumbua utaniambia asubuhi.”
“Sawa shem,” alijibu Aisha. Akamshika Bony na kumgeuzia kwake, akatoa ulimi kumwelekea, Bony akaudaka kwa sekunde kadhaa, akautoa, Aisha akampiga busu la kimyakimya, Bony akatoka. Ilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua.
Bony na mkewe walirudi chumbani, Bony akafikia kwenye kuoga…
“Unajua nilikwenda kule bila kuoga mke wangu,” alisema Bony, Neema hakumjibu, naye akaenda kuoga naye.
Waliporudi kitandani, Neema alikuwa na haya ya kusema kwa mume wake…
“Darling…”
“Naam…”
“Mimi simuelewi Aisha…”
“Kwa lipi tena baby?” aliuliza Bony kwa mshangao mkubwa huku akihisi tayari limesanuka…
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa, siku ya Ijumaa ijayo

Leave a Comment