×

Baba P… Baba Pili … Baba Pilima!-2

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:

“Sisi tunaishi Magomeni-Mwembechai!”
“He! Kwa hiyo wote ni Magomeni?”
“Ndiyo maana yake.”
“Watoto wako wanasoma wapi?”
“Watoto mtoto? Mimi nina mtoto huyohuyo mmoja tu…”
“Aaa! Noo bwana…nooo!”SASA JIACHIE MWENYEWE…

Mhudumu alitokea na kuingilia mazungumzo yao kwa kumuuliza baba Pili kama anataka kuongezea kinywaji…
“Tuongezee tafadhali,” alisema baba Pili…
Baada ya mhudumu kuondoka, waliendelea…

“Ina maana tunaweza kufanana kwa kila kitu kiasi hicho?” aliuliza baba Pili…
“Na mimi ndiyo nashangaa,” alijibu mama Pilima…
“Mh! Yaani hadi eneo la kuishi, yaani wote Magomeni?”
“Ndiyo hapo sasa.”

Moyoni baba Pili aliamini ile ndo’ ilikuwa fursa pekee ya kumnasa mwanamke huyo aliyeonekana kwake ana mvuto…
“Lakini kama mwingi wa habari…maana ukiona mwanamke unaongea naye na anakukodolea macho bila kufumbafumba, ogopa,” alijisemea moyoni mwanaume huyo.

Sasa wakawa kama marafiki waliojuana siku au miaka mingi sana. Walipiga stori nyingine za kifamilia na za nje ya familia. Za kifamilia zilikuwa hizi…
“Sasa mama Pilima, kama kuna baba Pilima unawezaje kutoka kukaa baa peke yako?” aliuliza baba Pili…

“Ah! Unajua ukifanya utafiti utagundua kuwa, wanaopenda kulewa, katika kila watu kumi, sita wana stresi zao, wanne tu ndiyo wanakwenda kwa matakwa yao…”
“Sasa wewe mama Pilima upo kundi gani?”
“La watu sita…teh! Teh! Teh!” alijibu mama Pilima na kucheka kidogo…
“Una stresi?”

“Ndiyo maana yake!”
“Zaidi ni nini?”
“Ah! Unajua tena mambo ya ndoa baba Pili…”
“Yamefanyaje?”
Mama Pilima akaachia tabasamu kidogo kisha akamwangalia baba Pili kwa macho ya mlegezo…

“Mambo ya aibu bwana,” alisema mama Pilima…
“Mh! Sisi wanandoa hatuna mambo ya aibu. Labda kama tungekuwa mabachela…teh! Teh! Teh!”

Mama Pilima aliamua kuachia ukweli kama kawaida ya wanawake…
“Unajua mimi na mume wangu, hata kuzaa ni kama Mungu tu…”
“Kwa nini iwe kama Mungu tu…”
“Ah! Yaani ningejua…wala…”
“Nini tena jamani mama Pilima?”

“Unajua mimi nilifunga ndoa bila kukutana kimwili na mume wangu…”
“Enhee..?”
“Tukiwa honeymoon ndiyo nikabaini tatizo…”
“Tatizo gani mama Pilima?” aliuliza baba Pili macho yote yakiwa kwenye uso wa mwanamke huyo ambaye katika kuongea alikuwa akibinua midomo, mara alegeze macho, mara aachie tabasamu la huba. Ilimradi tu!

“Nilishangaa sana, mume wangu alipoanza tu palepale akamaliza. Na mbaya zaidi akimaliza hawezi kuendelea tena mpaka upite mwezi na siku kadhaa…”
“Lo! Kweli hilo tatizo mama Pilima…”
“Umeona ee?”

“Basi bora angekuwa anasubiri hata dakika mbili, yaani yeye ni sekunde saba tu.”
“Sekunde saba!” alishangaa baba Pili…
“Ndiyo sekunde saba…siku nyingine hata kabla ya kuanza kwa mechi.”
Hapo baba Pili alijikuta akiangalia pembeni kwa aibu. Maana alimwona mama Pilima kama ameenda ndani sana. Halafu na yeye na vile alishamtamani, ikawa kwake ni kama anapunguziwa kazi…

“Lo! Kwa hiyo unahisi kulewa ndiyo sababu ya kukufanya uweje?”
Kwa kweli nikilewa, nikifika nalala zangu tu…teh Teh! Lakini nisipolewa, da! Namsumbua nikijua wazi kwamba, atanitesa tu.”
“Mimi naomba kukushauri,” alisema baba Pili. Mama Pilima akakaa mkao wa kusikiliza kwa undani zaidi…

“Enhe! Nasikiliza wazo lako baba Pili…”
“Badala ya kunywa pombe mpaka kulewa, ungetafuta wa pembeni ili awe mkata kiu yako,” alisema baba Pili huku akiangalia chini. Alijua si ushauri mzuri lakini kwa sababu yeye anafukuzia mzigo ilibidi aseme hivyo ili apime!
“Mh,” aliguna mama Pilima huku na yeye akiangalia upande mwingine kwa walipokuwa wamekaa wahudumu…

“Nimekukwaza kwa ushauri wangu mama Pilima?”
“Kwa kiasi fulani umenikwaza sana…”
“Kwa nini?”

“Sijawahi kusaliti na wala sipendi. Ingawa kama mwanamke naweza nikawa katika hali ya kujisikia kufanya hivyo lakini huwa najionya.”
Baba Pili alihema kwa nguvu na kumwangalia mwanamke huyo kisha akasema…
Je, nini kilitokea? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa, Ijumaa ijayo.

Leave a Comment