
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amethibitisha kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao, kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili National Hospital (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Akizungumza kuhusu msiba huo, Chacha amesema kifo cha kamanda huyo ni pigo kubwa kwa Jeshi la Polisi na wananchi wa Mkoa wa Tabora kutokana na mchango wake katika kuimarisha usalama na utulivu wa mkoa huo.
SACP Abwao alikuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kufariki dunia. Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ugonjwa wake na ratiba ya mazishi zinatarajiwa kutolewa na familia pamoja na mamlaka husika.
Viongozi mbalimbali wa serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wameendelea kutuma salamu za pole kufuatia kifo hicho, wakimkumbuka kama kiongozi aliyekuwa na weledi, nidhamu na kujituma katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.