Global TV inamtafuta Video Graphics Editor mwenye ubunifu, kasi na ujuzi wa kutengeneza maudhui ya kisasa yenye ubora wa hali ya juu kwa majukwaa ya kidijitali.
Sifa za Mwombaji
- Awe kijana wa kiume, mkazi wa Dar es Salaam.
- Awe na uzoefu wa kuandaa na kuhariri video, graphics na matangazo ya video.
- Awe na ujuzi wa kupiga picha za video kwa kutumia kamera za DSLR za aina mbalimbali kama Canon, Nikon, Sony, Panasonic, Fujifilm na nyinginezo.
- Awe na uzoefu wa kutumia Adobe Premiere Pro, Adobe After Effects, Adobe Photoshop, Canva, CapCut pamoja na programu nyingine zinazofanana.
- Awe na uwezo wa kutumia AI Tools kutengeneza na kuboresha picha, video na maudhui ya kidijitali.
- Awe na uelewa mzuri wa majukwaa ya YouTube, Instagram, Facebook, TikTok na mitandao mingine ya kijamii.
- Awe mbunifu, mwenye nidhamu, anayezingatia ubora wa kazi, anayependa kujifunza teknolojia mpya na anayeheshimu muda wa kukamilisha kazi (deadlines).
- Awe tayari kufanya kazi kwa ratiba zinazobadilika na kushirikiana vizuri na timu.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia barua pepe:
Mwisho wa kutuma maombi: 07 Julai 2026
Mawasiliano:
☎️ +255 799 444 036 (Office)
Ofisi:
📍 Global Group House, Mori Road, Dar es Salaam.
