×

Nandy na Billnass Waadhimisha Miaka Minne ya Ndoa Kwa Style ya Kipekee Goba, Dar – Picha

Usiku wa kuamika leo Julai 18, 2026 ulikuwa wa kipekee kwa mastaa wa Bongo Fleva, Nandy na Billnass, baada ya wawili hao kuadhimisha kumbukumbu ya miaka minne ya ndoa yao kwa sherehe ya kifahari iliyofanyika nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam.

Wawili hao walifunga ndoa Julai 16, 2022 jijini Dar es Salaam na tangu hapo wameendelea kuonyesha safari yao ya mapenzi mbele ya mashabiki.

Katika maadhimisho hayo, Nandy alionekana kupokea zawadi maalum kutoka kwa mume wake, Billnass, ambaye anadaiwa kumzawadia cheni aina ya Tiffany, zawadi iliyozua gumzo kwa mashabiki wao kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kupokea zawadi hiyo, Nandy alionekana kufurahia usiku huo wa mapenzi huku mashabiki wakitania kuwa siku hiyo alikuwa akila “dola tu” kutokana na namna ambavyo mume wake alivyompa heshima na zawadi za kipekee.

Kwa upande wake, Billnass naye alionekana kusherehekea kwa staili yake, huku akitania kuwa ameingia kwenye usiku huo kama “muuza madini wa Katoro” akimwaga zawadi na kuhakikisha kumbukumbu ya miaka yao ya ndoa inakuwa ya kipekee.

Nandy na Billnass wamekuwa miongoni mwa wanandoa maarufu kwenye tasnia ya burudani Tanzania, huku ndoa yao ikiwa imebarikiwa na mtoto wao wa kike, Naya.

Maadhimisho hayo yameonyesha tena ukaribu wao, huku wawili hao wakitumia nafasi hiyo kusherehekea upendo, mafanikio na safari yao ya miaka minne ndani ya ndoa.

Leave a Comment