
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mmoja na Wenyeviti wawili wa Bodi katika taasisi za umma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unahusisha viongozi wafuatao:
Salum Nassor Mnuna ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Prof. Esron Daniel Karimuribo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI).
Paul Peter Olekashe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).
Taarifa hiyo imetolewa Ikulu jijini Dar es Salaam leo Julai 21, 2026, na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Shaaban Kissu, kwa niaba ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
