
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia Julai 24, 2026, katika eneo la Mafiga, Manispaa ya Morogoro, kando ya barabara kuu ya Morogoro–Iringa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mtu mmoja amepoteza maisha huku watu wawili wakipata majeraha mbalimbali.
Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu, huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.