×

Peter Shalulile Atua Yanga Baada ya Kuondoka Mamelodi Sundowns

Yanga SC imemtambulisha mshambuliaji Peter Shalulile (32) raia wa Namibia kuwa mchezaji wake mpya, akijiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Mamelodi Sundowns kumalizika.

Baada ya taarifa hiyo, Mbunge wa Jimbo la Makete na shabiki wa Simba, Festo Sanga, alitoa utani akisema:

“Jirani mbona upo serious sana! Hutaki kabisa tubebe kombe? 😂 Shalulile mtu! 🤝”

Usajili wa Shalulile unatajwa kuwa miongoni mwa usajili mkubwa zaidi kuelekea msimu mpya na unatarajiwa kuongeza ushindani mkubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Leave a Comment