
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Ahmed Arajiga kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa Ngao ya Jamii 2026 kati ya Simba SC na Yanga SC.
Mchezo huo utachezwa kesho katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 2:30 usiku.
Arajiga atakuwa na jukumu la kusimamia mchezo huo unaowakutanisha watani wa jadi katika pambano la kuwania Ngao ya Jamii 2026.
