×

Mkesha wa Mwenge Buchosa, Polisi Sengerema Watoa Uhakika wa Usalama – Video

BUCHOSA, MWANZA — Jeshi la Polisi Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, limewahakikishia wananchi wa Buchosa kuwa litasimamia kikamilifu usalama wakati wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kufanyika katika eneo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa wa Polisi Wilaya ya Sengerema wakati wa fainali ya mashindano ya Mwenge Cup yaliyofanyika Buchosa.

Afisa huyo amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za mapema kuhusu viashiria vyovyote vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama kabla na wakati wa mkesha huo.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa maandalizi ya kiusalama yatazingatia kuhakikisha wananchi wanashiriki shughuli hiyo kwa utulivu na amani, huku hatua stahiki zikichukuliwa kudhibiti vitendo vinavyoweza kuvuruga usalama.

Mkesha wa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukutanisha wananchi mbalimbali wa Buchosa katika kushiriki shughuli za kijamii na kuadhimisha ujio wa Mwenge wa Uhuru katika eneo hilo.

Leave a Comment