×

St. Joseph’s College kuleta mapinduzi kitaaluma

UONGOZI wa Chuo cha St. Joseph’s College kilichopo Kihonda-Mizani, Morogoro kimejipanga kuleta mapimduzi makubwa katika kutoa ya elimu tofauti na vyuo mbalimbali visivyokuwa vya serikali.
Akizungumza na Gazeti la Amani, mkurugenzi wa chuo hicho, Seif Chomoka alisema kuwa St. Joseph’s imesajiliwa na Nacte kwa namba REG/BMG/046 na kina mazingira mazuri, walimu na nyenzo za kutosha ambazo zitamrahisishia mwanafunzi kupokea elimu ipasavyo.

“Elimu bora inatokana na mazingira, walimu wenye uzoefu, nyenzo na kadhalika, tumeboresha zaidi kwa lengo la kutoa elimu stahiki kwa wanafunzi wetu, tuna studio ya kisasa, huduma ya internet, hosteli nzuri zenye huduma za maji na umeme kwa saa 24, pia wanafunzi wetu tunawatafutia field katika ofisi za serikali na mashirika mbalimbali ya umma, kwa wale watakaofaulu vizuri chuo kitawatafutia pia ajira,” alisema Chomoka.

Nafasi za masomo chuoni hapo zipo wazi na wote wanakaribishwa. Chuo kinatoa nafasi za masomo katika kozi zifuatazo; Accountancy, Record Management, Business Administration, Information Technology, Procurement & Supply, Community Development, Human Resources Management, Early Childhood Education, Journalism & Mass Communication pamoja na Full Secretarial Course (Stage l&ll).

Aidha, Chomoka ametaja kuwa kozi hizo zitatolewa kwa ngazi ya Diploma kwa muombaji aliyehitimu kidato cha sita au mwenye cheti cha kozi yoyote kutoka vyuo vilivyosajiliwa na Nacte. Kwa upande wa masomo ya cheti ‘Certificate’ muombaji anatakiwa awe amehitimu kidato cha nne na kupata angalau alama ‘D’ mbili.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa simu namba, 0715257605, 0784257605 au  0769982572, barua pepe: [email protected]

Leave a Comment