
Mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Laurindo Dilson “Depu”, ameaga rasmi klabu ya Yanga pamoja na mashabiki wake baada ya kuondoka Tanzania na kurejea Angola.
Depu ametuma ujumbe wa kuwaaga mashabiki wa Yanga, huku akiwashukuru kwa mapokezi mazuri, upendo na ushirikano kubwa aliyopata tangu alipowasili klabuni hapo, pamoja na ushirikiano alioupata kutoka kwa wachezaji wenzake.
Akizungumza katika ujumbe wake, Depu amesema mashabiki wa Yanga wataendelea kubaki kwenye kumbukumbu zake, huku akisisitiza kuwa kuondoka kwake Tanzania si mwisho wa uhusiano wake na nchi hiyo.

“Kila mmoja wenu atabaki kwenye kumbukumbu zangu ninajisikia mwenye bahati sana kwa kila kitu nilichopata, hii si kwaheri, bali ni tutaonana hivi karibuni, asanteni sana, Tanzania,” amesema Depu
Depu alijiunga na Yanga SC Januari 2026 akitokea Radomiak Radom ya Poland, lakini baada ya kipindi kifupi akiwa na klabu hiyo, amerejea nchini Angola na kujiunga tena na Petro de Luanda.
Mshambuliaji huyo anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Petro de Luanda katika msimu ujao, huku akiwaacha mashabiki wa Yanga na kumbukumbu za kipindi chake kifupi ndani ya klabu hiyo.