
SHAHIDI WA TATU wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, Aman Sam Golugwa (Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA) leo Septemba 4, 2026 ameieleza Mahakama kuhusu mazingira ya mkutano wa chama uliofanyika Aprili 3, 2025, pamoja na madai mbalimbali yanayohusiana na kesi hiyo.
Akihojiwa na mawakili, Golugwa amesema Lissu hakushiriki katika maandalizi ya mkutano huo, ikiwa ni pamoja na kuwaita watia nia au kuwaalika waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa shahidi huyo, wakati maandalizi ya mkutano huo yakifanyika, Lissu alikuwa katika Operesheni ya CHADEMA iliyokuwa ikiendelea Kanda ya Nyasa yenye kaulimbiu ya “No Reforms, No Elections”.

Golugwa amesema yeye mwenyewe aliwasiliana kwa simu na baadhi ya viongozi wakuu wa chama, akiwemo Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Saidi pamoja na Naibu Katibu Mkuu, kuwaeleza kuhusu uwepo wa mkutano huo.
Amesema waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walialikwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, ambaye pia ni mjumbe wa Sekretarieti.

Shahidi ameitajia Mahakama baadhi ya vyombo vya habari alivyokumbuka kuwepo katika mkutano huo kuwa ni Clouds TV, Jambo TV, Chanzo TV, ITV na Gazeti la Mwananchi.
Golugwa amesema hakukuwa na masharti maalumu wala maelekezo yaliyotolewa kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kutekeleza majukumu yao katika mkutano huo.
Pia amesema kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja kutoka katika mkutano huo, akivitaja Jambo TV na Chanzo TV kuwa miongoni mwa vyombo vilivyorusha matangazo hayo.
Kuhusu madai kwamba Tundu Lissu ndiye aliyerushaa matangazo hayo kupitia Jambo TV, Golugwa amekanusha na kusema madai hayo ni “uongo na upotoshaji”.
Aidha, amesema maneno yaliyochapishwa na Jambo TV yalichapishwa na mwandishi wa habari wa chombo hicho aliyekuwa amealikwa katika mkutano huo, na kwamba Lissu hakuhusika katika kuyachapisha.

GOLUGWA: HAKUKUWA NA MANENO YA KUCHOMA VITUO
Katika sehemu nyingine ya ushahidi wake, Golugwa amekanusha kuwepo kwa maneno yaliyodaiwa kuhusu kuchoma vituo vya mwendokasi au vituo vya kupigia kura.
Akiulizwa kuhusu maneno aliyosomewa mahakamani, shahidi amesema hakuna sehemu aliyosikia ikisema “tutachoma vituo vya mwendokasi” wala “tutachoma vituo vya kupigia kura”.
Pia amesema katika maneno hayo hakukuwa na kauli inayomtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
RIPOTI ZA WAANGALIZI
Golugwa pia amehojiwa kuhusu ripoti za waangalizi wa uchaguzi alizozitaja katika ushahidi wake.
Amesema ripoti hizo ni za mwaka uliopita na kwamba yeye alizitafuta na kuzihifadhi, lakini hakuzifikisha mahakamani.
Ameeleza kuwa ripoti hizo zimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza na kukiri kuwa yeye si mwandishi wa ripoti hizo.
Katika mahojiano hayo, shahidi amesema hana elimu ya sheria, lakini amedai kuwa hata mtu asiye na utaalamu wa sheria anaweza kuzungumza mbele ya mahakama.
Kuhusu uwezo wake wa kutafsiri ripoti kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, Golugwa amesema tafsiri isiyo sahihi inaweza kuathiri maana ya ripoti, ingawa amesema si lazima kueleza kiwango chake cha ufaulu wa Kiingereza.
GOLUGWA AKANUSHA KUWA NA IMANI NA RIPOTI NZIMA YA JAJI CHANDE
Katika sehemu nyingine, shahidi amesema hana imani na ripoti yote ya Jaji Chande, lakini amesisitiza kuwa baadhi ya mambo aliyoyazungumza mahakamani yana msingi katika kile alichokielewa mwenyewe.
Ameeleza pia kuwa hakumbuki baadhi ya taarifa zilizohusiana na ripoti za waangalizi, ikiwemo majina au vichwa vya baadhi ya ripoti alizoulizwa.
MALALAMIKO YA UCHAGUZI
Golugwa ameiambia Mahakama kuwa hakuwahi kujaza wala kuwasilisha fomu za kugombea nafasi yoyote katika uchaguzi huo.
Amesema malalamiko aliyoyazungumza mahakamani yalihusu wagombea na kwamba malalamiko hayo yaliwasilishwa katika mamlaka husika pamoja na kamati za rufaa.
Alipoulizwa kama malalamiko hayo yalipelekwa mahakamani baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya kamati za rufaa, Golugwa amesema hawakuona haja ya kwenda mahakamani kwa sababu, kwa mtazamo wao, “mambo ya kisiasa tunamaliza kisiasa”.
GOLUGWA: WATAZAMAJI WA KIMATAIFA WALIPINGA KESI YA UHAINI
Katika ushahidi wake kuhusu kesi inayomkabili Lissu, Golugwa amesema baadhi ya watazamaji wa kimataifa walionyesha masikitiko kuhusu kufunguliwa kwa kesi hiyo.
Kwa mujibu wa ushahidi wake, watazamaji hao walidai kuwa hawakuona mazingira ya uhaini katika maneno yaliyotajwa kuwa yalizungumzwa na Lissu na walitaka aachiliwe bila masharti.
Pia amesema Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lilieleza kuwa kukamatwa kwa Lissu hakukuwa halali na kwamba shtaka dhidi yake lilikuwa na lengo la kumuumiza kisiasa.
Golugwa pia amedai kuwa kikao cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola kilieleza kuwa kesi hiyo ilikuwa ya kisiasa na kuitaka Lissu aachiliwe bila masharti.
SABABU ZA VIFO NA MAUAJI
Akijibu swali kuhusu sababu zilizotolewa na Jaji Mkuu kuhusiana na mauaji yaliyotokea, Golugwa amesema kwa kumbukumbu zake sababu hizo zilihusisha madai ya Katiba Mpya, masuala ya utekaji na watu kupotea pamoja na manung’uniko ya muda mrefu ya wananchi ambayo hayakuwa yametatuliwa.
Ushahidi wa Golugwa unaendelea katika Mahakama, huku upande wa utetezi ukiendelea kumuuliza maswali kuhusu mkutano wa Aprili 3, 2025, maandalizi yake, ushiriki wa Lissu na maudhui ya maneno yanayohusishwa na kesi hiyo.
Ignas: Nimesikia ulikuwa kampeni meneja na hukugombea nafasi yoyote ile
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Kwa hiyo ulipata hizo taarifa kwa watu wengine
Golugwa: Kwa kuwa nilikuwa karibu na wagombea nilikua naona kila kitu
Iganas: Unatambua matokeo ya uchaguzi ngazi ya ubunge 2020 yanapingwa mahakamani na yapi mlishinda
Golugwa: Kama nilivyosema chaguzi hizi siwezi kukumbuka ni malalamiko mangapi
Ignas: Je jambo lolote ambalo mliwasilisha mahakamani na mahakama ikaona hoja zenu zina msingi
Golugwa; Sikumbuki
Ignas: Unaweza sasa kuiambia hapa kuwa hoja ulizoleta hapa mahakamani hazikuwa na msingi na hivyo zipuuzwe
Golugwa: Hapana ni hoja za msingi
Ignas: Kwa kuwa umelamikia swala la madiwani embu tuambie ni kata ngapi malalamiko yenu yalithibitisha ni sahihi
Golugwa: Kwenye ngazi ya mahakama sina idadi
Ignas: Utakubaliana nami malalamiko yenu hayakuthibitishwa na mahakama?
Golugwa: Sio kweli yalikuwa ni ya kweli
Ignas: Ni mashauri mangapi mliwasilisha mahakamani
Golugwa: Hakuna
Ignas: Mahakamani hamkupeleka
Golugwa: Uchaguzi ni swala la kisiasa
Ignas: Hebu tuambie ya kwamba ni maneno ya kusikia na kamati za rufaa zilikubali malamiko yao yalikuwa na shida
Golugwa: Yote yalitupiliwa mbali
Ignas: Sababu hayakuwa na mashiko
Golugwa: yalitupiliwa mbali sababu ya uhuni na ushenzi
Mambo ya kisiasa tunamaliza kisiasa – Golugwa
Maswali ya Dodoso kwa shahidi namba tatu Aman Sam Golugwa
Ignas: Ni kweli hukujaza wala kuwasilisha fomu za kugombea katika mamlaka husika
Golugwa: Sikujaza fomu yoyote ya kugombea
Ignas: Ni kweli kwamba hukuwasilisha fomu
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Ni kweli kwamba malamiko uliyoleta hapa mahakamani yalikuwa yanahusu wagombea
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Malamiko uliyosema hapa mahakamani umeyapata toka vyanzo vingine
Golugwa: Sio kweli
Ignas: Mtu akiwa na malalamiko anapeleka wapi
Golugwa: Kwenye mamlaka husika
Iganas: Inamaana hujui wapi malamiko yanapopelekwa
Golugwa: Anapaswa kupelekea pale anapogombea na kwenye kamati ya rufaa
Ignas: Mlishinda mangapi
Golugwa: Yalitupiwa mbali sababu ya ushenzi niliosema
Ignas: Mliwasilisha hayo malalamiko yenu mahakamani
Golugwa: Tuna tambua ila hatukuona haja ya kwenda mahakamani
Ignas: Inamaana mlirudhika na maamuzi ya kamati za rufa:
Golugwa: Hapana mambo ya kisiasa tunamaliza kisiasa
Ignas: Kwenye zile kanuni za uchaguzi kuna sehemu ulikutana na neno mkwe wa rais
Golugwa: Hakuna
Ignas: Umeileza mahakama umewahi kukamatwa na hujawahi kufunguliwa hati ya mashitaka mahakamani
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Ni kweli baada ya kusikilizwa polisi walikuachia
Golugwa baada ya mimi kutoa maelezo
Ignas: Na mara ya pili unasema ulikamatwa tarehe nane mwezi wa kumi na moja napo uliachiwa baada ya kusikilizwa maelezo yako
Golugwa: Ni kweli
Ignas: Umeleza elimu yoyote uliyonayo juu ya sheria
Golugwa: Sina elimu yoyote ya sheria
Ignas: Sasa umepata wapi ujasiri wa kuieleza mahakama mambo ya kisheria
Golugwa: Hata Layman anaweza kuongea na yuko mbele yako
Ignas: Ulieleza kuhusu ripoti za waangalizi ni za mwaka gani
Golugwa: zote ni za mwaka jana
Ignas: Wewe ni custodian wa hizo ripoti
Golugwa: Nilitafuta na kuzihifadhi
Ignas: Umezileta hapa mahakani
Golugwa: Hapana
Ignas: Hizo ripoti zipo kwa lugha gani
Golugwa: kwa kiingereza
Ignas: Utakubaliana na mimi wewe sio muandishi wa hizo ripoti
Golugwa: Ndio mimi sio muandishi wa hizo ripoti
Ignas: Hao walitoa ripoti kuna siku walikuita uzifasiri toka kingereza kwenda kiswahili
Golugwa: Kwanini na kwa sababu gani ni tafsiri
Ignas: Wewe hapa mahakamani umezielezea kwa kiswahili
Golugwa: Ndio
Ignas: Utakubaliana na mimi wewe form four ulipata grade gani kingereza
Golugwa: Sikumbuki
Ignas: Unatatizo la kumbukumbu
Golugwa: Ikihitajika ku refresh memory
Ignas: Je unafahamu mtu akifasiri inaweza kuharibu maana ya ripoti
Golugwa: Kama mtu akitafsiri vibaya yanaweza kuathiriwa au yasiathiriwe
Ignas: Umeelaza juu ya uwezo wako kwenye lugha ya kiingereza
Golugwa: Sio lazima
Ignas: Unafasiri document za kiingereza
Golugwa: Kingereza ulipata nini Golugwa C au D
Ignas: Sasa na D yako unataka kutafsiri ripoti kubwa kama hizi?
Golugwa: Ina shida gani
Ignas: Haya tuambie title ya ripoti ya Thabo mbeki kwa kiIngereza ilisemaje
Golugwa: Kwa kweli sikumbuki
Ignas: Tuje ile ripoti ya SADC wewe mfasiri inaitwaje
Golugwa: Kwa kingereza sikumbuki ila inazungumzia
Iganas: Kwa kingereza bwana wewe si mkalimani
Golugwa: Sikumbuki
Ignas: Uliweza kufuatiliwa ripoti ya waangalizi wa Jumuiya ya Afrika mashariki
Golugwa: Hapana
Ignas: Tukirudi kwenye hii ripoti ya Jaji Chande uliizungumzia jana swali langu ni kwamba una imani na ripoti hii
Golugwa: Sina imani nayo
Ignas: Kwa hiyo hata kile ulicho kieleza jana huna imani nacho licha kuwa kwenye ripoti ya Jaji Chande
Golugwa: Sikubaliana na wewe nilichokueleza mimi nina imani nacho licha kwamba sina imani na ripoti yote
Ignas: Inamaana kuna ambavyo vilikupendeza wewe
Golugwa: Hapana kitu gani hicho kuzungumzia
Ignas: Hebu turudi kwenye kikao cha watia nia uliongea habari ya unyunyu na makapi kulikuwa na habari ya manukato kwemye kikao chenu cha watia nia
Golugwa: Haikuwepo
Ignas: Waheshimiwa mimi nimemaliza watafuata wenzangu.