×

Puma Energy Yazindua Ziara ya PumaGas Mikoa Mitano Nchini

Dar es Salaam, 3 Septemba 2026: Puma Energy Tanzania imeanza rasmi ziara ya PumaGas itakayopita katika mikoa mitano nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kusogeza huduma za gesi ya kupikia karibu na wananchi na wafanyabiashara.

Ziara hiyo imezinduliwa katika kituo kipya cha Puma Energy kilichopo Bunju, Dar es Salaam, na itaendelea kwa kipindi cha wiki nane katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma na kuhitimishwa rasmi jijini Mwanza.

Kupitia ziara hiyo, Puma Energy inalenga kuwafikia watumiaji wa gesi ya kupikia katika maeneo mbalimbali, kuwapa nafasi ya kupata taarifa kuhusu matumizi ya gesi, kujifunza zaidi kuhusu bidhaa na huduma zinazopatikana, pamoja na kuwasiliana na mawakala wa PumaGas katika maeneo yao.

Ziara hiyo inabeba ujumbe wa kampeni yao ya “Hakuna Kuchochea, Tumerahisisha na PumaGas,” unaolenga kuzungumzia namna gesi ya kupikia inavyoweza kutumika katika shughuli za kila siku za kaya na biashara.

“Lengo letu si kuwaambia watu kuhusu gesi ya kupikia pekee, bali kuwapa nafasi ya kuifahamu, kuona namna inavyotumika na kupata taarifa wanazohitaji kabla ya kufanya uamuzi. Kwa kupeleka PumaGas moja kwa moja kwenye jamii, tunataka kuwa karibu zaidi na wateja wetu na kuelewa mahitaji yao katika maeneo mbalimbali,” alisema Bi. Lilian Kanora, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Puma Energy Tanzania.

Katika maeneo yatakayofikiwa, timu za PumaGas zitakutana na kaya, wafanyabiashara wa chakula, migahawa, hoteli pamoja na mawakala wa gesi. Kutakuwa pia na maonesho ya matumizi ya gesi na fursa kwa wananchi kuuliza maswali kuhusu matumizi, upatikanaji na ujazaji wa gesi kwenye mitungi.

Kwa upande wa wafanyabiashara wanaotumia gesi katika shughuli zao za kila siku, ziara hiyo itatoa nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu matumizi ya gesi katika biashara kama vile mama ntilie, watoa chipsi, migahawa na hoteli. Mawakala nao watashirikishwa katika kuimarisha upatikanaji wa bidhaa na huduma kwa wateja katika maeneo yao.

Safari hiyo itafikia kilele chake Mwanza, ambapo Puma Energy itaingia rasmi katika soko la Kanda ya Ziwa. Uzinduzi huo utahusisha hafla ya kutambulisha PumaGas katika soko hilo, kukabidhi mtungi kwa mteja wa kwanza na kumtambua wakala wa kwanza wa PumaGas katika eneo hilo, pamoja na kushirikisha wadau na vyombo vya habari.

Sehemu ya uzinduzi katika Mkoa wa Mwanza pia itahusisha maonesho ya matumizi ya gesi katika shughuli za kawaida za kila siku. Mama ntilie atapika chapati kwa kutumia mtungi wa PumaGas, huku wananchi wakipata nafasi ya kuona moja kwa moja kiasi cha chakula kinachoweza kuandaliwa kwa kutumia gesi hiyo.

Kwa Puma Energy, ziara hii ni sehemu ya mpango mpana wa kuongeza upatikanaji wa gesi ya kupikia na kuifikisha huduma hiyo kwa wananchi katika maeneo mengi zaidi nchini.

Kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza, ziara hiyo itachukua wiki nane kuzunguka jamii mbalimbali, kusikiliza mahitaji ya watumiaji na kuwasogezea huduma za PumaGas karibu zaidi na maeneo wanayoishi na kufanya biashara.

PumaGas: Hakuna Kuchochea, Tumerahisisha.

Leave a Comment