×

Rais Samia Awashukuru Wananchi kwa Salamu na Dua Baada ya Kifo cha Mumewe

Paul Makonda, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akimfariji, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa shukrani kwa wananchi wa ndani na nje ya nchi pamoja na makundi mbalimbali kwa salamu za pole, dua na maombi waliyomfikishia yeye na familia yake kufuatia kifo cha mumewe, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, kilichotokea Zanzibar Septemba 7, 2026.

Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais Samia amesema yeye pamoja na familia yake wameguswa sana na upendo, mshikamano, salamu za pole, dua na maombi waliyoyapokea katika kipindi hiki cha majonzi.

Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.

Rais Samia amewashukuru Waku wa Nchi na Serikali, viongozi wa kitaifa, wanadiplomasia, jumuiya ya kimataifa, viongozi wa dini pamoja na Watanzania wote kwa salamu, dua na faraja zao katika kipindi chote cha majonzi hadi leo, ambapo wanaendelea kuomboleza kifo cha mpendwa wao.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Zanzibar tarehe 7 Septemba 2026, na kuacha familia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi cha majonzi.

Baadhi ya Viongozi wa Timu za Yanga na Simba wakimfariji Dkt. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.
Mke wa Rais wa Msumbiji Gueta Selemane Chapo akimfariji, Dkt. Samia.
Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akimfariji Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Balozi Amina Salum Ali akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mama Siti Mwinyi akimfariji Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mama Zakia Meghji akimfariji, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi akimfariji, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.

Leave a Comment