Dk.Shein Azindua Rasmi Jengo La Abiria Uwanja Wa Ndege Zanzibar
Global Publishers September 28, 2020 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa jengo la Abiria la (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,hafla iliyofanyika leo Kisauni Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja (kulia kwa Rais) Mgombe wa Urais Zanzibar Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi),
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amezindua rasmi jengo jipya la abiria (Terminal III) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume leo Septemba 28.
Ujenzi wa jengo hilo linaloitwa Terminal III lenye uwezo wa kubeba idadi kubwa ya abiria, ulilenga kuongeza kipato kupitia wasafiri na watalii mbalimbali watakaoingia na kutoka Visiwani Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa jengo la Abiria la (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,hafla iliyofanyika leo Kisauni Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja (kulia) Mgombe wa Urais Zanzibar Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi)akifuatiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xe Xiaowu .
Katika kuzindua jengo hilo, Rais Shein alielezea mafanikio mbalimbali ambayo uongozi wake wa awamu ya saba umeyafanya na manufaa ambayo Zanzibar watayapata
“Katika mtizamo wa hivi leo, lengo la kuwa na miundombinu mizuri na usafiri imetanuka zaidi kwa kuzifanya nchi zinazoendelea ziweze kupiga hatua kubwa kwa kuvutia fursa mbalimbali za kiuchimi ikiwemo watalii na wawekezaji” alisema Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Ujenzi,Usafirishaji na Mawasiliano Mhe. Sira Ubwa Mamboya (katikati) wakipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd,Mustafa Aboud Jumbe (wa pili kulia) alipokagua jengo la Abiria la (Terminal III) baada ya ufunguzi rasmi uliofanyika leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, Kisauni Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja (kushoto)Meneja wa Ujenzi Jengo Nd.Yasser De Costa
Rais Shein ameeleza pia serikali ya Zanzibar imefanikiwa kulipa dola za Marekani milioni 31 ambao ni fedha za mkopo waliotumia kujenga kituo hicho.
Pia wamefanikiwa kumaliza kulipa dola za Marekani milioni 58 walizofanyia marekebisho bila kutegemea mkopo huku akieleza iwapo bajeti itapigwa vizuri Zanzibar itafanya mambo makubwa bila mikopo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein( katikati) akiwapungia mkono wananchi katika hafla ya Ufunguzi wa jengo la Abiria la (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,hafla iliyofanyika leo Kisauni Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja (kulia kwa Rais ) Waziri wa Ujenzi,Usafirishaji na Mawasiliano Mhe. Sira Ubwa Mamboya
“Tumeamua tutajitegemea wenyewe kwenye mambo ya msingi lazima tufanye wenyewe hii kukopa kopa tunajichelewesha lakini tukipanga bajeti yetu vizuri tutafanya mengi” alisema.
Msanii wa kizazi kipya Asley akiwaburudisha wananchi na Viongozi waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa jengo la Abiria la (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,hafla iliyofanyika leo Kisauni Wilaya ya Magharibi (B) Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Rais Shein aliwaomba wananchi waliohudhuria ufunguzi huo kumchagua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Hussein Mwinyi kama mtu sahihi wa kusimamia miradi iliyopo Zanzibar katika Serikali ijayo.