ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefanya uteuzi wa Katibu wa Baraza la Wawakilishi na Wajumbe wawili wa Baraza hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Septemba 14, 2026, na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mansura M. Kassim, uteuzi huo umehusisha viongozi watatu.
Katika uteuzi huo, Ndugu Hassan Ali Hassan ameteuliwa kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi. Kabla ya uteuzi huo, Hassan alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uandishi wa Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Aidha, Ndugu Nassor Ahmed Mazrui na Ndugu Omar Said Shaaban wameteuliwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Septemba 14, 2026.
Viongozi walioteuliwa wanatarajiwa kuapishwa mbele ya Baraza la Wawakilishi Septemba 16, 2026.

