Mfanyabiashara maarufu nchini, Jennifer Bilikwija, anayefahamika zaidi kwa jina la Niffer, amezungumzia suala la mahusiano na namna ambavyo mtu anaweza kukabiliana na hali ya kuchezewa na mwenza wake.
Niffer amesema kuwa kuchezewa katika mahusiano huku mtu akiwa anafahamu kinachoendelea kunaweza kuwa tofauti na pale ambapo anasalitiwa bila kutarajia.
“Kuchezewa kwenye mahusiano huku unajua unachezewa hakuumi, ila ukichezewa bila kutarajia unaweza kufa,” amesema Niffer.
Katika kauli yake, Niffer amesisitiza umuhimu wa mtu kuwa makini na kutambua hali halisi ya uhusiano wake, badala ya kuishi bila kujua kinachoendelea nyuma yake.
“Jifunze kujua mwenyewe kama unachezewa ili ujue namna ya kucheza,” ameongeza.
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni mtazamo wa Niffer kuhusu namna watu wanavyopaswa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika mahusiano, huku akisisitiza umuhimu wa kutambua mapema mwenendo wa mwenza.
Ujumbe wake umeibua mjadala kuhusu uaminifu katika mahusiano na namna ambavyo mtu anavyoweza kuathirika pale anapogundua usaliti ambao hakutarajia.