×

Rais Samia Apokea Hati za Utambulisho za Mabalozi sita Ikulu, Dar leo – Picha

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Salem Yousef Alhamdan, Balozi Mteule wa Kuwait hapa nchini, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 13 Oktoba, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Oktoba 13, 2026, amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi sita wateule wanaoiwakilisha Kuwait, Nigeria, Ujerumani, Ubelgiji, Sweden na Falme za Kiarabu (UAE), katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mabalozi waliowasilisha hati hizo ni Salem Yousef Alhamdan wa Kuwait, Rahmat Omobolanle Mohammed wa Nigeria, Annett Gunther wa Ujerumani, Lot Debruyne wa Ubelgiji, Ingrid Johansson wa Sweden na Mohamed Salem Ahmed Al Rashdi wa Falme za Kiarabu.

Rais Samia, akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Rahmat Omobolanle Mohammed Balozi Mteule wa Nigeria.

Hafla hiyo ni sehemu ya taratibu za kidiplomasia zinazowaruhusu mabalozi wateule kuwasilisha rasmi hati zao za utambulisho kwa mkuu wa nchi wanayokwenda kuiwakilisha.

Kupitia hatua hiyo, mabalozi hao wanatarajiwa kutekeleza majukumu yao ya kidiplomasia nchini Tanzania kwa mujibu wa taratibu na kanuni zinazotawala mahusiano kati ya mataifa.

Tukio hilo linaakisi mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi hizo sita, ambazo zinashirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maslahi ya pamoja.

Rais Samia, akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Annett Gunther, Balozi Mteule wa Ujerumani.
Rais Samia, akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Lot Debruyne Balozi Mteule wa Ubelgiji.
Rais Samia akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Ingrid Johansson, Balozi Mteule wa Sweden.
Rais Samia akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mohamed Salem Ahmed Al Rashdi, Balozi Mteule wa Falme za Kiarabu (UAE) 

Leave a Comment