×

Rais Samia Ateua Viongozi Watatu, Atengua Uteuzi wa Mkuu RC Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi watatu katika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, Oktoba 28, 2026.

Katika uteuzi huo, Bi. Angeline Lubala Mabula ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Bw. Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Aidha, Bw. Dunford George Mpelumbe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu ambaye amemaliza muda wake. Kabla ya uteuzi huo, Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika uteuzi mwingine, Bw. Omar Ali Omar ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huo, Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Omar anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Khamis Hamad ambaye amemaliza muda wake. Hata hivyo, tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatangazwa baadaye.

Leave a Comment