×

Akilimali: Wazee Yanga Tunampigia Dua Ajibu

 

KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amemtaka mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu kufanya kazi katika klabu hiyo bila ya presha yoyote kwa kuwa wazee wapo nyuma yake kuhakikisha wanamsapoti.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Akilimali alisema kuwa wanamkaribisha Ajibu kwa mikono miwili aweze kukipiga katika klabu yake hiyo mpya ya Yanga na kudai kuwa wazee wa klabu hiyo wanampa sapoti kubwa na watakuwa nyuma yake.

 

“Tunafurahi na tunamkaribisha kama kijana wetu, tunamtakia kila la kheri, wazee tupo pamoja naye afanye kazi asiwe na wasi, sisi tunamuombea dua aweze kufanya vyema na kuitumikia timu yake aliyokuwa na mapenzi nayo tangu siku nyingi.

 

“Ajibu hapa Yanga ajisikie yupo nyumbani, afanye kazi na acheze mpira, tunaamini uwezo huo anao,” alisema Akilimali.

Khadija Mngwai na Said Ally | CHAMPIONI

Leave a Comment