×

Rais Samia na Rais wa Angola Wapanda Mti wa Kumbukumbu Dodoma

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipanda mti wa kumbukumbu pamoja na mgeni wake João Manuel Conçalves Lourenço (Picha ya chini), Rais wa Jamhuri ya Angola katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 30 Oktoba, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepanda mti wa kumbukumbu pamoja na Rais wa Jamhuri ya Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço, katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, leo Oktoba 30, 2026.

Kitendo hicho kimefanyika ikiwa ni sehemu ya shughuli za ziara ya Rais Lourenço nchini Tanzania, ambapo viongozi hao wameendelea kushiriki matukio mbalimbali ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Awali, Rais Samia na mgeni wake walipokea heshima ya nyimbo za mataifa yao katika uwanja wa gwaride, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Baada ya shughuli hizo, Rais Samia alimsindikiza na kuagana na Rais Lourenço katika uwanja huo, kufuatia ziara yake nchini Tanzania.

Ziara hiyo inaendelea kuonesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Angola pamoja na dhamira ya kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali yenye manufaa kwa mataifa hayo mawili.

Leave a Comment