×

MultiChoice Tanzania Yazindua Kampeni Mpya ya “Pata Zaidi”

MultiChoice Tanzania leo imezindua kampeni yake mpya ya “Pata Zaidi” , ikitangaza maboresho makubwa zaidi kuwahi kufanyika kwenye huduma ya DStv nchini Tanzania.
Katika maboresho hayo, vifurushivya DStv vimerahisishwa, punguzo kubwa la bei, maudhui mengi zaidi ya Kitanzania, chaneli mpya ya SuperSport Swahili pamoja na fursa mpya kwa wabunifu na wasanii wa Tanzania.
Uzinduzi huo unaonesha dhamira ya MultiChoice Tanzania ya kuendelea kutoa thamani zaidi kwa wateja wake huku ikiwekeza katika ukuaji wa sekta ya ubunifu nchini, kuimarisha matumizi ya Kiswahili na kukuza simulizi za Kitanzania.
Kiini cha mabadiliko hayo ni marekebisho makubwa ya vifurushi vya DStv ambapo idadi ya vifurushi vya msingi imepunguzwa kutoka sita hadi vinne, hatua inayorahisisha uchaguzi wa kifurushi kulingana na mahitaji, maslahi na uwezo wa kifedha wa mteja.
Miongoni mwa maboresho makubwa yaliyotangazwa leo ni:
Vifurushi vya DStv sasa vitakuwa vine badala ya Sita
Wapenzi wa michezo sasa wataweza kupata maudhui ya michezo kupitia kifurushi kipya cha DStv Sports kwa TSh 50,000 tu, kutoka bei ya awali ya TSh 118,000.
Mashabiki wa Ligi Kuu ya England sasa wataweza kufurahia mechi za EPL kupitia kifurushi kipya cha DStv Select kwa TSh 25,000 pekee, badala ya TSh 68,000 za kifurushi cha Compact cha zamani.
Wapenzi wa maudhui ya nyumbani hususan tamthilia, vichekesho, filamu na kadhalika, sasa watapata katika kifurushi kipya cha Starte Sh 15,000 badala ya bei ya zamani ya Sh 27,500.
Maudhui mengi zaidi ya Kiswahili na yanayozalishwa Tanzania yataendelea kuongezwa kwenye majukwaa ya DStv ikiwemo tamthilia kabambe ya KARATA itakayoanza mwezi Novemba 2026.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Tanzania Sophie Tchatchoua alisema mabadiliko hayo yameongozwa na ujumbe mmoja muhimu kwa wateja: ‘TUMEWASIKILIZA’
“MultiChoice tunaamini kuwa DStv inapaswa kukua na kubadilika pamoja na wateja wetu. Kwa miaka mingi tumekuwa tukisikiliza kwa makini maoni yao. Wametueleza wanahitaji thamani zaidi, uchaguzi rahisi, unyumbufu zaidi na maudhui yanayoakisi maisha na mambo yanayowahusu. Maboresho haya ni jibu letu kwa maoni hayo.”
“Tumewasikiliza, na ndiyo maana tumefanya marekebisho makubwa ya vifurushi vyetu ili viwe rahisi kueleweka na viendane zaidi na mahitaji ya makundi tofauti ya wateja. Tumevipunguza kutoka vifurushi sita hadi vinne vya msingi ili kurahisisha uchaguzi kwa wateja.”
“Tumewasikiliza, na ndiyo maana tumepunguza kwa kiwango kikubwa bei za vifurushi vyetu. leo shabiki wa michezo aliyekuwa analipa TSh 118,000 ataweza kufurahia michezo kwa TSh 50,000 tu.
Mashabiki wa EPL sasa wanaweza kupata ligi hiyo kwa TSh 25,000. Tunataka wateja wetu wapate maudhui mengi zaidi, uchaguzi mpana zaidi na thamani bora zaidi kwa kila shilingi wanayotumia.” Alisisitiza Sophie
“Tumewasikiliza, wapenda burudani na tamthilia, na ndiyo maana tunawaletea KARATA, tamthilia ya asilimia 100 ya Kitanzania iliyoundwa na Watanzania kwa ajili ya Watanzania. Hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuendelea kukuza sekta ya ubunifu nchini na kuonesha vipaji vya kipekee tulivyonavyo.”
Katika hatua kubwa kwa tasnia ya utangazaji wa michezo Afrika Mashariki, MultiChoice Tanzania imezindua SuperSport Swahili, chaneli mpya itakayotoa matangazo na uchambuzi wa michezo ya kiwango cha dunia kwa lugha ya Kiswahili.
“Tumewasikiliza, wapenzi wa michezo, na ndiyo maana tunazindua SuperSport Swahili ili kuwapa fursa ya kufurahia michezo ya kiwango cha kimataifa pamoja na uchambuzi wake kwa Kiswahili.”
“Tumewasikiliza, wazazi ambao wametuomba tuongeze maudhui ya ndani yenye kuelimisha watoto. Ndiyo maana tunawaletea Ubongo Kids kwenye DStv, ili watoto wapate maudhui ya kujifunza na kuburudika kwa wakati mmoja kwa lugha ya Kiswahili.”
Kampeni ya “Pata Zaidi” ni zaidi ya mabadiliko ya vifurushi. Ni uthibitisho wa dhamira ya MultiChoice Tanzania ya kuweka mteja mbele, kuwekeza katika sekta ya ubunifu nchini, kukuza Kiswahili na kusimulia hadithi za Kitanzania kwa ubora wa kimataifa.
“Mwisho wa yote, jambo hili linahusu kumuweka mteja mbele. Linahusu kuwapa thamani zaidi, uchaguzi zaidi na uzoefu wa kutazama unaoakisi maisha ya Watanzania wa leo. Tunawashukuru wateja wetu kwa uaminifu wao, maoni yao na kwa kuendelea kuwa sehemu ya safari hii. Kwa sababu msingi wa mabadiliko haya ni kauli moja rahisi: “Tumewasikiliza.” Alihitimisha Sophie.

Leave a Comment