Kijana mdogo, Benjamin Semzaba, anafikishwa mbele ya mkono wa sheria akikabiliwa na kesi nzito ya mauaji. Baada ya kunguruma kwa kipindi kirefu, hatimaye kesi iliyokuwa inamkabili inaelekea kufika mwisho na hukumu kutolewa.
Ushahidi wote umeshakamilika na hakuna shaka kwamba Ben ndiye aliyeua kwani ukiachilia mbali ushahidi huo, yeye mwenyewe mara kwa mara amekuwa akikiri kwa kinywa chakekufanya mauaji hayo.
Wakati kila mtu akiamini kwamba Ben ameua, Jordan Rwechungura, wakili aliyekuwa akimtetea katika kesi hiyo ambaye ukiachilia mbali kazi yake pia alikuwa rafiki mkubwa wa Ben, waliyecheza pamoja tangu wakiwa watoto wadogo, anakuwa mgumu kuamini kwamba ni kweli rafiki yake huyo ameua.
Historia ya makuzi ya Ben, inamfanya Jordan ahisi kwamba Ben hajaua ila ameamua kukubali kwa sababu ambazo yeye mwenyewe ndiye anayezijua. Jitihada zake za kutaka kuufahamu ukweli zinagonga mwamba kutokana na Ben kukataa kutoa ushirikiano, muda wote aking’ang’ania kwamba ni yeye ndiye aliyeua.
Hatimaye siku ya hukumu inawadia, Ben akiwa amedhoofika sana na kubadilika kutokana na mateso ya gerezani, anahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia.
Upande wa pili, historia ya maisha ya Ben inaelezwa, tangu akiwa kijana mdogo kabisa, akiishi na mama yake pamoja na wadogo zake, Mtaa wa Maporomoko kwenye mji mdogo wa Tunduma.
Licha ya maisha ya kifukara anayopitia, anaonesha uwezo mkubwa darasani, anafaulu kwa kiwango cha juu na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Mzumbe ambako nako anaendelea kung’ara. Anarudi nyumbani kwao baada ya shule kufunga lakini anashtuka baada ya kukuta watu wengi nje ya nyumba yao.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…Kijana mdogo, Benjamin Semzaba, anafikishwa mbele ya mkono wa sheria akikabiliwa na kesi nzito ya mauaji. Baada ya kunguruma kwa kipindi kirefu, hatimaye kesi iliyokuwa inamkabili inaelekea kufika mwisho na hukumu kutolewa.
Ushahidi wote umeshakamilika na hakuna shaka kwamba Ben ndiye aliyeua kwani ukiachilia mbali ushahidi huo, yeye mwenyewe mara kwa mara amekuwa akikiri kwa kinywa chakekufanya mauaji hayo.
Wakati kila mtu akiamini kwamba Ben ameua, Jordan Rwechungura, wakili aliyekuwa akimtetea katika kesi hiyo ambaye ukiachilia mbali kazi yake pia alikuwa rafiki mkubwa wa Ben, waliyecheza pamoja tangu wakiwa watoto wadogo, anakuwa mgumu kuamini kwamba ni kweli rafiki yake huyo ameua.
Historia ya makuzi ya Ben, inamfanya Jordan ahisi kwamba Ben hajaua ila ameamua kukubali kwa sababu ambazo yeye mwenyewe ndiye anayezijua. Jitihada zake za kutaka kuufahamu ukweli zinagonga mwamba kutokana na Ben kukataa kutoa ushirikiano, muda wote aking’ang’ania kwamba ni yeye ndiye aliyeua.
Hatimaye siku ya hukumu inawadia, Ben akiwa amedhoofika sana na kubadilika kutokana na mateso ya gerezani, anahukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia.
Upande wa pili, historia ya maisha ya Ben inaelezwa, tangu akiwa kijana mdogo kabisa, akiishi na mama yake pamoja na wadogo zake, Mtaa wa Maporomoko kwenye mji mdogo wa Tunduma.
Licha ya maisha ya kifukara anayopitia, anaonesha uwezo mkubwa darasani, anafaulu kwa kiwango cha juu na kuchaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Mzumbe ambako nako anaendelea kung’ara. Anarudi nyumbani kwao baada ya shule kufunga lakini anashtuka baada ya kukuta watu wengi nje ya nyumba yao.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
“
Pole na safari Ben, karibu nyumbani lakini kuna matatizo kidogo, hebu njoo huku tuzungumze, mzee Mpogo, jirani yao na mwenyekiti wa mtaa waliokuwa wanaishi, alimdaka Ben juujuu na kusogea naye pembeni.
Akawaita baadhi ya vijana waliokuwa nje ya nyumba hiyo na kuwaelekeza kumpokea Ben mizigo yake na kuipeleka nyumbani kwa mzee huyo, Ben akazidi kupigwa na butwaa.
“Kama unavyoona, watu wamekusanyika hapa kwenu kwa sababu kuna tatizo,” alisema mzee huyo kwa sauti ya upole na kumtaka Ben awe mvumilivu katika kipindi hicho kigumu.
“Kwani kuna nini? Si uniambie tu? Halafu mbona nasikia kama watu wanalia huko ndani?” alisema Ben huku uvumilivu ukionesha kuanza kumshinda, ilibidi mzee Mpogo amueleze ukweli kwamba mdogo wake wa mwisho, Mwivano alikuwa amefariki dunia baada ya kuugua ghafla.
“Mungu wangu, Mwivano kafariki? Haiwezekani, haiwezekani! Nasema haiwezekaniiiii,” Ben alipaza sauti na kuanza kuangua kilio kwa nguvu, akamponyoka mzee Mpogo na kukimbilia hadi ndani kwao ambako alikuta wanawake wengi wakiwa wamekaa chini sebuleni kwao, wote wakiomboleza.
Aliwapita na kuingia mpaka chumbani ambako alimkuta mama yake na baadhi ya majirani, wakiwa wanalia kwa uchungu huku mwili wa mdogo wake, Mwivano ukiwa umelazwa kwenye kitanda kichakavu kilichokuwa ndani ya chumba hicho.
“Mwivano! Mwivano! Amka mdogo wangu, nimekuletea zawadi kutoka Morogoro,” alisema Ben, kauli iliyoamsha vilio upya ndani ya nyumba hiyo, Ben akawa anaendelea kulia huku ameikumbatia maiti ya mdogo wake, baadaye akahamia pale chini mama yake alipokuwa amekaa akiwa hajiwezi kwa kulia, akamkumbatia na wote wakawa wanaendelea kulia kwa uchungu.
Baadaye mipango ya mazishi ilianza kufanywa, kwa kuwa hawakuwa na fedha za kwenda kuuhifadhi mwili mochwari, ilibidi maiti ilazwe humohumo ndani mpaka siku ya pili ambapo mazishi yalifanyika kwenye Makaburi ya Maporomoko.
Kilichomuumiza zaidi Ben, ni kuona maisha ya mdogo wake huyo yamekatishwa kwa sababu ya umaskini kwani alishikwa na homa kali ya ghafla na kwa sababu ya kukosa fedha, mama yake alishindwa kumpeleka hospitali. Badala yake akamchemshia muarobaini na kumnywesha, homa ikazidi kuwa kali, baadaye akaanza kutapika na kuharisha mfululizo mpaka alipofikwa na mauti.
“Huenda ilikuwa ni malaria ya kawaida tu ambayo kama angepelekwa hospitali angepona,” alisema Ben wakati wakirejea nyumbani baada ya mazishi.
“Ukilaumu sana unakuwa unakufuru mwanangu, kazi ya Mungu haina makosa japo roho inauma sana.”
“Muda mwingine tunamsingizia Mungu mama, basi limeshatokea hatuna cha kufanya,” Ben alikuwa akizungumza na mama yake, huku machozi yakiendelea kumtoka kwa wingi. Lilikuwa pigo kubwa sana kwake, alimpenda sana mdogo wake huyo na hata alipokuwa akirudi nyumbani, alikuwa amembebea zawadi kadhaa.
Siku zilizidi kusonga mbele, taratibu wanafamilia wote wakaanza kusahau kilichotokea na kuchukulia kila kitu kuwa cha kawaida. Ben hakutaka kuacha asili yake, baada ya mambo ya msiba kumalizika, alianza kwenda sokoni kufanya vibarua vya kubeba mizigo kama kawaida, akawa anaisaidia familia yake huku na yeye pia akiweka fedha kwa ajili ya matumizi atakapokuwa shuleni.
Hatimaye likizo iliisha, Ben akaanza maandalizi ya kurejea shuleni ambapo siku moja kabla ya kuondoka, alienda kulitembelea kaburi la mdogo wake, akamuombea dua kisha akapitia kwa mwalimu wake, Tung’ombe ambaye alimpa tena fedha za ada na za matumizi yake kama alivyoahidi.
Alfajiri na mapema ya siku iliyofuatia, safari ya kuelekea Morogoro ilianza, japokuwa mama yake Ben bado alikuwa anaumwaumwa, alimsindikiza mwanaye mpaka stendi ya basi baada ya kuwa wameshafanya maombi maalum ya kumtanguliza Mungu amsimamie katika safari yake na katika masomo yake.
Ben akasafiri kwa basi la New Force mpaka Morogoro ambako aliwasili salama na kwenda moja kwa moja mpaka shuleni, akawa ni miongoni mwa wanafunzi wa mwanzo kuripoti shuleni. Siku chache baadaye akayaanza rasmi masomo ya kidato cha sita, ukiwa ndiyo mwaka wake wa mwisho kabla ya kuhitimu elimu ya sekondari.
Kila alipokuwa anakumbuka kifo cha mdogo wake kilichosababishwa na ufukara wa familia yake, Ben alikuwa akipata uchungu mkali ndani ya moyo wake uliomsukuma kusoma kwa bidii ili siku moja aje kuiokoa familia yake. Siku zilizidi kusonga mbele, akazidi kuongeza bidii kwenye masomo na kama ilivyokuwa awali, kila mtihani ulipokuwa unakuja, alikuwa akiongoza na kuwaacha wenzake kwa tofauti ya alama nyingi.
Siku zilizidi kuyoyoma na hatimaye, Ben na wanafunzi wengine wote walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita, huku kila mmoja akimtabiria Ben makubwa. Baada ya kumaliza mitihani, Ben na wanafunzi wengine waliohitimu masomo yao, walitawanyika, kila mmoja akarudi nyumbani kwao.
Ben alifunga tena safari mpaka nyumbani kwao, Tunduma ambako alipokelewa na hali ya umaskini kama aliyoiacha, akajiingiza rasmi kwenye shughuli ndogondogo za kujiingizia kipato lakini tofauti na miaka ya nyuma, safari hii aliamua kufanya kazi ya kufundisha, akapewa nafasi ya kufundisha kwenye shule aliyosomea, Tunduma Sekondari huku akilipwa fedha za kujikimu kutokana na kazi hiyo. Alianzisha pia masomo ya ziada (tuition) ambapo wanafunzi wengi walikuwa wakisoma kwake kutokana na jinsi alivyokuwa anafundisha vizuri. Japokuwa alikuwa amehitimu kidato cha sita, alikuwa na uwezo mkubwa wa kufundisha kuwazidi hata walimu waliosomea kabisa kazi hiyo.
Fedha alizokuwa anapata, kwa kiasi kikubwa zilimsaidia sana yeye na familia yake, wakawa hawahangaiki tena kuhusu mahitaji madogomadogo ya familia, ikiwemo chakula.
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumamosi kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi.
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW
INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/
TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari
FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers
YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1