Na Mwandishi Wetu
MASTAA kibao wakiwemo, mtangazaji Millard Ayo, mwanamuziki Hellen George ‘Ruby’, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine kibao wanatarajiwa kujumuika pamoja katika Tamasha la Mimi ni Nani? Shtuka Mapema linalotarajiwa kufanyika Aprili 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Josam House, Mwenge jijini Dar.
Akizungumza na Risasi Vibes, mratibu wa tamasha hilo, Harris Kapiga alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwakusanya wale wote kuanzia waliomaliza kidato cha nne na hawakufanya vizuri kisha kuwapa somo la kutokata tamaa, kwanza wajitambue wao ni kina nani na pili waweze kushtuka mapema.
“Tunatarajia kuwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda sambamba na Lilian Mwasha na Angel Magoti ambapo mbali na hiyo tamasha hili ni kuwainua wale wote waliokata tamaa ya maisha waweze kujitambua mapema,” alisema Harris na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa watu wawili.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.