ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:
“Darling, yule fundi anasema kamaliza lile gauni na kesho anakwenda Tanga. Ngoja niende mara moja…Nancy nakuja baada ya dakika ishirini,” Neema alimwambia mumewe na Nancy, akasimama na kwenda kuchukua sendozi, akatoka.
Ile anafunga mlango tu, Nancy akamdaka Bony…
“Shemeji mi sikubali…”
SHUKA NAYO MWENYEWE SASA…
“Hukubali nini tena shemeji?” aliuliza Bony huku akiwa ameshakumbatiwa…
“Ameenda wapi Neema?”
“Kuchukua gauni?”
“Wapi?”
“Kule mtaa wa mwisho.”
“Anaweza kutumia dakika ngapi kwenda na kurudi?”
“Kama nusu saa hivi…kuna nini kwani Nancy.”
“Kumbe huyu demu niliyemkuta hapa anaishi hapa? Kwa nini hukuniambia? Kumbe mnamsaliti Neema hivihivi kweupe?”
“Shem labda umesahau tu, nilikwambia yale ya kule si ya kumwambia Neema. Itakuwa tabu kubwa kwenye ndoa yangu.”
“Mimi shem leo nitasema. Kama nisingemkuta humu ndani sawa lakini kumkuta ni tatizo. Yaani Neema amekubali kumpa hifadhi halafu ndiyo shukurani zake hizi? Hii si sawasawa hata kidogo.”
Bony alianza kuwa mpole. Aliamini Nancy atasema na akisema kweli itakuwa tabu.
“Shem, kwani unasemaje wewe?”
“Unaniachaje na mimi? Nilikuuliza kule kwani mimi sina sifa ya kunifanya wewe unitongoze? Ukasema ninazo, sasa nioneshe.”
“Sasa hivi?”
“Ndiyo, si umesema Neema atatumia nusu saa kwenda na kurudi?”
“Lakini Nancy si unajua ndani humu kuna yule dada…”
“Kwa hiyo unamwogopa siyo?”
“Heshima tu.”
“Heshima wakati tayari mmeshaivunja wenyewe?”
“Oke, je akitokea na kutukuta katika hali hii?”
“We wasiwasi wako uko wapi?”
“Si atamwambia Neema?”
“Kwa hiyo na mimi nimwambie?”
“Basi Nancy, sasa unatakaje?”
“Mimi sijui, wewe ndiyo mwenyeji wangu kwenye nyumba hii,” Nancy alimwambia Bony huku akiangalia huku na kule kama anayetafuta mahali pa kufanyia jambo fulani.
“Sikia basi, ukienda mbele kule, mlango wa kulia ni wa chumbani kwangu, kushoto ni wa chumba cha wageni, mbele kule ni kwa yule shemeji anayeishi hapa. Sasa wewe nenda kaingie mlango wa kushoto wa chumba cha wageni.
Nancy aliondoka kama baruti, akaenda kuzama kwenye chumba hicho. Bony akaangalia mazingira akamfuata.
Aliingia kwa umakini sana ili asijenge maswali kwa Aisha aliyekuwa amelala chumbani kwake.
“Chapuchapu…chapuchapu Bony,” alisema Nancy akijua madhara ya kujiachia ndani ya chumba kile.
Uzuri ni kwamba, Nancy alipozamana tu akajichojoa nusu uwanja. Kwa hiyo, akakutwa yuko ‘stendbai’ kwa mpira.
Bony alipoambiwa chapuchapu hakulaza damu. Akatimiza ahadi na himizo. Ikawa chapuchapu..!
Nancy alikuwa akijizuia kwa kutumia nguvu nyingi kuhakikisha kwamba anapiga kelele za ishara badala ya uhalisia kwani angetumia uhalisia sauti ingetoka. Bony kwa vile alijua yupo kwenye chapuchapu alimsikilizia Nancy ambaye alipotulia tu na yeye akamaliza mpambano.
Nancy alijiweka sawa, akajikausha akaomba kutoka…
“Naweza kutoka? Kuko kwema huko kweli?” aliuliza kwanza Nancy…
“Ngoja nitoke mimi kwanza,” alisema Bony, akafungua mlango kutoka.
Kufika sebuleni, akamtumia meseji Nancy ambaye simu yake ilikuwa sailensi, naye akatoka. Anafika tu sebuleni, Aisha anafungua mlango na kutoka chumbani.
Alifika sebuleni, akakaa akiwasalimia kwa kuwaambia za muda. Wakaitika wote. Lakini cha ajabu, Aisha alikwenda kukaa kwenye kochi la kukaa watu wawili ambapo Bony alitangulia kukaa. Nancy akashangaa sana kwani kochi kubwa lilikuwa halina mtu na yeye Nancy alikaa kochi la mtu mmoja…
“Vipi mume wangu?” Aisha alimwita Bony mume mbele ya Nancy. Nancy alishtuka sana, akakaa sawasawa na kumtumbulia macho akijiandaa kusema lolote juu ya wito huo…
“Khaa! We anti, kwani huyo si shemejio, unamwitaje mumeo wakati unajua ana mke wake ni kwa nini lakini au kuna kitu gani kati yenu?” aliuliza Nancy huku akimwangalia Bony aone atasema nini na atachukuliaje kwenye kule kuitwa ‘…mume wangu?’
Kabla ya jibu lolote lile kutoka kwa Aisha au Bony kujibu kwa wito, Neema alisikika akiingia huku akiimba nyimbo za dini.
Ujio huo wa Neema ulimfanya Nancy amwangalie Aisha kama anayesema…
“Hilo limefumaniwa sasa tuone… na mimi nitakupa vipande vyako.”
Neema aliingia sebuleni, Nancy akamfuata kwa macho anavyoingia akitarajia kumwona akishtushwa na kitendo cha wawili hao kukaa kochi moja la watu wawili wakati kuna kochi kubwa la watu watatu na halina mtu huku yeye akijifanya ni shoga mwema sana kwa Neema…
“He! Jamani…nawaona mke na mume mmekaa wenyewe mmependazaje?” alisema Neema huku akionesha kuwa hana wasiwasi wowote na wala tukio lile kwake si ishu…
Aisha alimtumbulia macho Nancy yale ya kumsuta kama anayemwambia…
“Sema lingine sasa, mwenye mali mwenyewe amekubali we mpambe utafanya nini?”
“Nakwambia…nimetoka kulala namkuta mume anahangaika peke yake hapa sebuleni, mke mkubwa kachepuka,” alisema Aisha huku macho yakiwa kwa Nancy…
“Neema,” Nancy aliita kwa suati ya mshtuko huku akisimama kwa jaziba…
“Niambie shoga yangu, nilifuata gauni langu kule mbele,” alisema Neema akienda kukaa kwenye lile kochi kubwa lisilokuwa na mtu…
Je, unajua nini kilitokea? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.