Stori: Mwandishi wetu
Tukio lililotikisa wiki hii kwenye ulimwengu wa burudani Bongo ni pamoja na wizi uliotokea juzikati maeneo ya Ununio jijini Dar ambapo wasanii mbalimbali walikuwa kwenye shooting ya video ya Mheshimiwa Sugu ambaye ni mkongwe kwenye game.
Ilikuwa mida ya usiku ambapo magari ya watu mbalimbali waliokuwepo kwenye tukio hilo likiwemo la Prodyuza Master J yalivunjwa vioo kisha vikaibwa vitu mbalimbali.
Master alipigwa waleti yake iliyokuwa na mkwanja, begi lililokuwa na ‘dokumenti’ za ofisni kwake ikiwemo laptop pamoja na begi lililokuwa na nguo ambapo mwenyewe anasema vitu hivyo vina thamani ya kama shilingi milioni nne. Pole Master J.