Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakipaza sauti zao kudai mafao yao.
….Wakitafakari kujua hatma yao.
…Wakihojiwa na baadhi ya wanahabari waliofika kwenye tukio hilo.
….Wafanyakazi hao wakiwa nje ya ofisi zao zilizopo eneo la Victoria jijini Dar.
Mahojiano yakiendelea.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Ulinzi ya Optima jijini Dar es Salaam, jana waliandamana katika ofisi zao zilizopo Victoria jijini Dar wakishinikiza kulipwa mshahara wa mwezi uliopita pamoja na kujua kama baadhi yao wataendelea kufanya kazi na kampuni hiyo kutokana na baadhi ya mashiriki waliyokuwa wakiyafanyia kazi kusitisha mikataba na kampuni yao.
Kamera yetu ilifanikiwa kufika ofisini hapo na kukuta wafanyakazi hao wakiwa nje ya ofisi zao ambapo kwa mujibu wa malalamiko yao walidai kuwa kuwepo kwao nje kunatokana na madai yao ya mshahara wa mwezi wa tatu kutokulipwa pamoja na hatma ya ajira yao.
Akijibu malalamiko hayo, mkurugenzi wa oparesheni wa kampuni hiyo, Mwaikambo Abdul alikiri kuwepo na madai hayo ambayo alisema ni ya kweli.
“Tunafahamu madai yao, ni ya kweli, kilichosababisha kucheleweshwa mshahara huo ni kutokana na lampuni kubwa jijini Dar waliyokuwa wakifanyanayo kazi kusitisha mkataba na kusababisha kampuni yetu kuyumba, lakini tutahakikisha mafao yao tunawalipa,” alisema Mwaikambo.
NA DENIS MTIMA/GPL