×

Rock City wamsubiri Ne-Yo kwa hamu

ne-yo-non-fiction

 Shaffer Chimere Smith ‘Ne-Yo

MKALI wa Muziki wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Chimere Smith ‘Ne-Yo’ anatarajiwa kushuka Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza maarufu kama Rock City na kupiga shoo ya ‘live’ kwa kutumia vyombo.
Akizungumza na Showbiz, mmoja wa waratibu wa shoo hiyo iliyopewa jina la Jembeka Festival 2016, Michael ‘DJ Kflip’ alisema kuwa wakazi wa jijini hapo wanaonekana kuwa na shauku kubwa ya kumshuhudia mkali huyo akifanya yake jukwaani na bila shaka siku hiyo itakuwa ni ya kuvunja rekodi kwa watu watakao hudhuria.

“Neyo atatua na timu nzima ya watu 22, watu wa Rock City wanaonakana kuwa na shauku sana, ninauhakika siku hiyo atavunja rekodi,” alisema DJ Kflip.

Katika shoo hiyo, staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond naye atakuwepo kumsindikiza Ne-Yo huku mastaa kibao wa Bongo Fleva kutoka Dar na Mwanza watakinukisha jukwaani.

Shoo hiyo imedhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers

Leave a Comment