Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa kuhutubia mkutano wa hadhara Aprili 10, 2016.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa (jina halikupatikana) akimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aipohutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo, Aprili 10, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwendesha pikipiki maarufu na hodari, Zaina Amour wa kijiji cha Nandagara wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakizungumza na mwendesha pikipiki maarufu na hodari, Zaina Amour wa kijiji cha Nandagara wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)