Ukitaka kumjua mwanamke mmbeya ‘shakunaku’ utamjua tu. Kwanza kama likitokea tukio yeye anakuwa ni msimuliaji mkuu. Akipewa ofa ya kilevi, akishakunywa bia mbili tu atatoa siri zote za jirani na maeneo yote yanayomzunguka.
Huwa hapendi marafiki ambao siyo wambeya. Akizungumza anapenda awe anasikilizwa yeye tu, ukimbishia anaweza hata kurusha ngumi. Kwake kutukana matusi ya nguoni ni kawaida, ikitokea adui yake kashindwa jambo, atahakikisha analisambaza mtaa mzima. Kwanza huwa ni maskini na kama ana watoto, atafanya kila liwezekanalo ashindane na wenye nazo.
Aidha, huwa makini kufuatilia kila tukio linalotokea mtaani kwake ili kwenda kuwaambia wengine tena kwa kuongeza na chumvi kulipa uzito. Huyo ndiye mwanamke mmbeya.