×

Nay wa Mitego Ajipa Dili la Kuosha Gari Zake

Stori: Musa Mateja

Kama ulikuwa ukidhani kuwa Mwanamuziki Nay wa Mitego ni bishoo, utakuwa umechelewa sana kwani jamaa amejipa dili ya kuosha gari zake kisha pesa ambayo angemlipa muoshaji anaiweka kwenye waleti yake.

Akipiga stori na safu hii, Nay alisema mara nyingi huchukulia kuosha magari yake kama sehemu ya kufanya mazoezi hivyo haoni shida kujipa dili hilo.

“Kuosha magari yangu wala sioni shida, kuna siku naamka asubuhi sana na kuifanya kazi hiyo kwa umakini, kwani kuna tatizo gani kujipa dili hilo siku mojamoja,” alihoji msanii huyo mwenye mafanikio makubwa kwenye gemu la muziki.

Leave a Comment