×

Queen Suzy: Eti shing’ ngapi, nani kasema tunajiuza?

Stori: Hamida Hassan
Mnenguaji wa muda mrefu wa Muziki wa Dansi nchini, Queen Suzy amewajia juu wanaume wakware wanaodhani mabinti wanaofanya kazi hiyo wanajiuza akidai kuwa, usumbufu wanaopata ni mkubwa.

Bishosti huyo alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye Kipindi cha Girlstalk cha Star TV ambapo alisema, amekuwa akishangazwa na wanaume wanaowatunza pesa kwa staili ya kuwawekea kwenye matiti na makalioni, jambo ambalo linawafanya wajisikie vibaya.

“Hili ni tatizo, unakuta mtu anakuja kukutuza jukwaani, eti mpaka akuwekee kwenye sehemu zako za siri, au mwingine ukimaliza shoo anakuambia eti amevutiwa na jinsi ulivyokuwa unacheza hivyo anataka muondoke wote, halafu anakuuliza eti shing’ngapi, nani kasema tunajiuza?” alihoji mwanadada huyo ambaye kwa sana anaitumikia Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma.’

Leave a Comment