Wachezaji wa Norwich wakiwa hoi baada ya kushushwa daraja kutoka EPL.
Klabu ya Norwich City imeshushwa daraja kutoka Ligi ya Kuu ya Uingereza licha ya ushindi wa bao 4 – 2 dhidi ya Watford usiku wa kuamkia leo.
Ushindi wa Sunderland wa 3-0 dhidi ya Everton Jumanne uliwafikisha hadi alama 38 na kwa kuwa Norwich na Newcastle hawawezi kuwafikia, moja kwa moja klabu hizo mbili zikashushwa daraja.
Kwa sasa Norwich wana alama 34 sawa na Newcastle. Klabu nyingine iliyoshushwa daraja ni Aston Villa iliyo na alama 17 kwa sasa.Baada ya kushushwa daraja, Norwich sasa watakuwa wakichezea tu fahari mechi yao ya mwisho dhidi ya Everton Jumapili. Watford watajaribu kumaliza msimu vyema dhidi ya Sunderland nyumbani.

