Miss Albino 2016 ambaye ni mlemavu wa ngozi, Evelyn Felix, akimpa mkono Naibu Waziri Katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Ajira, Bunge, Vijana na Walemavu Dkt. Adallah Possy.
Evelyn (kulia) akimpa mkono Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, katika maadhimisho hayo.
Risala ikisomwa kwa mgeni rasmi, Abdallah Possy.
Meza kuu wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa.
Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya ya IPP, Dkt. Reginald Mengi akizungumza jambo wakati wa kilele hicho.
Baadhi ya maalbino wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikisomwa kwa mgeni rasmi.
Hapa baadhi wakifanya biashara zao katika mabanda yaliyokuwepo viwanjani hapo.
Evelyn (katikati) akiwa na warembo wenzake ambao ni mshindi wa pili na wa tatu.
Baadhi ya watu mbalimbali wakipiga picha ya pamoja na Evelyn.
NAIBU Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Ajira, Bunge, Vijana na Walemavu, Dkt. Abdallah Possy, ameongoza kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kuongeza Uelewa Kuhusu Ualbino jijini Dar es Salaam iliyoanza Juni 11 wiki iliyopita.
Maadhinisho hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar ambapo Possy ndiye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo.
Katika maadhimisho hayo pia viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, alihudhuria hafla hiyo ambapo nasaha mbalimbali juu ya kuwathamini watu wenye ualbino zilitolewa, ikiwemo juu ya makundi maovu yanayofanya vitendo vya kuwaua.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Haki ya Ujumuishi, Haki ya Ushiriki Watoto Wenye Ualbino Wasikilizwe na Walindwe’.
NA DENIS MTIMA/GPL
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz
