Stori: Gladness Mallya
STAA wa kibao cha Moyo Mashine, Benard Paul ‘Ben Pol’ amesema hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa, kwani hayadumu.
Akiteta na mtandao huu, Ben Pol alisema mastaa wengi hawana mapenzi ya kweli, kwani hayatoki moyoni kwa vile aliwahi kuwa na uhusiano na mmoja wapo, lakini penzi lao halikudumu hata miezi miwili.
“Mimi siyo mpenzi sana wa kuwa na uhusiano na mastaa, nimeshajaribu mara moja lakini haukudumu, hivyo niko
na mtu wa kawaida tu kwa sababu mapenzi ya mastaa hayatoki moyoni,” alisema Ben Pol.
