Kama unasumbuliwa na muwasho wa ngozi au madhara yoyote yaliyoikumba ngozi yako tiba ya mwanzo nyumbani kwako ambayo inaweza kukusaidia ni hii hapa.
Mafuta ya chai ‘Tea Tree Oil’
Mafuta ya chai ni mazuri kwa kutibu muwasho wa ngozi pamoja na kulinda ngozi na bakteria washambuliaji.
Juisi ya kitunguu swaumu na kitunguu maji
Chukua vitunguu vyote visage kwa pamoja upate juisi yake kisha upake eneo linalokuwasha, juisi hiyo husaidia kuondoa muwasho wa ngozi uliosababishwa na bakteria.
Glasi ya maziwa ukichanganya na bizari ya manjano
Kunywa glasi ya maziwa freshi vuguvugu yaliyochanganywa na bizari ya manjano kijiko kimoja cha chai, kunywa kila siku mpaka utakapoona hali hiyo imeisha.
Maziwa mgando na siki ya tufaha
Chukua maziwa mgando ‘Yogurt’ changanya na siki ya tufaha kulingana na tatizo ulilonalo, inaweza kuwa unawashwa mwili mzima au mkono tu inategemea na wewe unatumiaje lakini ukishachanganya maziwa na siki hiyo paka mwili mzima.
Bila shaka wenye tatizo la muwasho wa ngozi tiba hii ya asilia itawasaidia muhimu ni kufuata maelekezo.
asante kwa ushauli